Header Ads


Tetesi za Usajili leo jumatano ya Tarehe 16.8.2017


BARCA YAKATAA KUMSAJILI MAHREZRiyad Mahrez Leicester City
Barcelona wameikataa fursa ya kumsajli Riyad Mahrez kutoka Leicester City, kwa mujibu wa TransferMarketWeb .


MAN CITY YAMTOLEA OFA ALEXISAlexis Sanchez Arsenal
Manchester City wanajipanga kutoa kitita cha £60 millioni kwa ajili ya nyota wa Arsenal Alexis Sanchez kwa mujibu wa  The Telegraph .


PEREZ ANATAKA KUONDOKA ARSENALLucas Perez Arsenal
Lucas Perez yu mbioni kukamilisha uhamisho wake kutoka Arsenal siku chache zijazo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 11 kurejea Deportivo La Coruna, kwa mujibu wa  Daily Mail. 


CHELSEA YAMTAKA COSTA KUREJEA MAZOEZINIAntonio Conte Diego Costa
Diego Costa anayetaka kuondoka Chelsea ameambiwa arejee kwenye mazoezi ya klabu hiyo ikiwa anataka kupata nafasi kwenye kikosi cha Antonio Conte, kwa mujibu wa habari kutoka The Sun .


BARCA YAMTENGEA HAZARD €120MEden Hazard, Chelsea
Barcelona wanataka kumsajili Eden Hazard kutoka Chelsea kwa adai ya uhamisho ya euro milioni 120 majira haya ya joto, kwa mujibu wa Diario Gol .
Real Madrid pia wanataka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji lakini Barca bado wanalo tumaini la kuishawishi Chelsea kumuuza.


BARCA KUONGEZA OFA YA COUTINHOHD Coutinho
Barcelona hawatakata tamaa kumsajili Philippe Coutinho na wapo tayari kutoa dau nono la paundi milioni 137 kuishawishi Liverpool kufanya biashara, limeripoti Sun .
Miamba hao wa Catalan wamechachamaa wakitaka kumsajili mchezaji huyo tangu kuondoka kwa Neymar, lakini Liverpool bado wakingali kusita kumuuza.


ASENSIO KUIZUNGUMZIA ARSENAL KWENYE MKUTANO WA DHARURAMarco Asensio Eibar Real Madrid LaLiga 04032017
Mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio atafanya mazungumzo ya dharura na klabu yake kuhusu uhamisho kwenda Arsenal, kwa mujibu wa  The Mirror .
Gunners wanapambana kufikia dau la paundi milioni 72 kumsajili Muhispania huyo, lakini bado pia yumo kwenye rada za Manchester United, City na Liverpool na Barcelona pia lakini atabaki Bernabeu ikiwa atapewa mkataba mpya.


WILSHERE ATAKIWA NEWCASTLEJack Wilshere, Arsenal, Premier League, 20160508
Newcastle United wamejipanga kumsajli mchezaji wa Arsenal ambaye amekosa ushawishi Emirates Jack Wilshere kwa mujibu wa  Sun .


MBAPPE KUIGHARIMU PSG ZAIDI YA NEYMARKylian Mbappe Monaco
Paris Saint-Germain wipata saini ya Kylian Mbappe kutoka Monaco kwa bei kubwa kuliko ile ya Neymar, limeripoti The Times.
Miamba hao wa Ligue 1 walitumia euro milioni 220 kumsajli Neymar kutoka Barcelona.
Post a Comment
Powered by Blogger.