Steven Gerrard Amesema Kuna Umuhimu wa Kumsainisha Van Dijk - Mtazamo News: Home

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

TANGAZO


Tuesday, August 22, 2017

Steven Gerrard Amesema Kuna Umuhimu wa Kumsainisha Van Dijk

Kocha wa Liverpool U18 Steven Gerrard amesema kuna umuhimu wa Livepool kumsainisha mlinzi wa kati wa Southampton Virgil van Dijk ili kuweza kuendana na kasi ya ushindani katika mashindano msimu huu.

Gerrard  alisema anahisi kuwa ili Jurgen Klopp aweze kufurahia msimu wa mafanikio huko Liverpool  anapaswa kumsajili beki huyo ambaye amekuwa na kipaji kikubwa uwanjani na ambaye anajua nini anatakiwa kukifanya awapo uwanjani.

 Aliiambia BT Sport: "Ndio [yeye ni lazima]. "Kwa ajili yangu, ikiwa unataka kushindana katika ligi na katika Ligi ya Mabingwa (Van Dijk anahitajika). "Timu ipo vizuri  lakini bado tunahitaji saini mbili au tatu ndani."

TANGAZO