Nahitaji Mfamasia Awe Anaprinti Karatasi Yenye Kuonyesha Dawa Zilizopo Kwenye Stoo Yake- Ummy Mwalimu - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 20 August 2017

Nahitaji Mfamasia Awe Anaprinti Karatasi Yenye Kuonyesha Dawa Zilizopo Kwenye Stoo Yake- Ummy Mwalimu

 Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa hospitali inayomilikiwa na Kanisa ya inayoitwa Dkt.Artiman iliyopo manispaa ya sumbawanga,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt.Khalfan Haule na kuliani ni Afisa Tawala wa  Mkoa wa Rukwa Bernard Makali
 Msimamizi wa hospitali hiyo sister Yasinta Rugabo akisoma taarifa ya hospitali hiyo
Na.WAMJW-Rukwa   
Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wametakiwa kusimamia fedha za dawa pamoja na upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwenye mkoa huo

Waziri wa Afya,naendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati akiongea na viongozi na watumishi wa Wilaya na mkoa wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapa

Nahitaji mfamasia awe anaprinti karatasi yenye kuonyesha dawa zilizopo kwenye stoo yake ili mganga anayeingia zamu siku hiyo aweze kujua dawa zilizopo na kumuandikiamgonjwa wake kuliko kuanmdika dawa ambazo hazipo kituoni hapo

Aidha Waziri Ummy aliwapongeza mkoa huo kutokana na kuwa na hali nzuri nya uwepo wa dawa katika vituo vyote alivyotembelea ingawaje bado kuna changamoto ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu uchangiaji wa dawa na kuwataka wakimaliza dawa walizonazo stoo zikiisha wanatakiwa kupunguza bei za dawa ili wananchi waweze kupata dawa hizo pasina shaka

Mheshimiwa Rais alisema hataki kuona wananchi wanapata shida ya upatikana wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali hivyo akaongeza bajeti ya dawa kwa miaka miwili mfululizao?akitolea mfano kwa mkoa wa Rukwa ,mwaka 2016/2017 bajeti ya dawa iliongezeka kutoka milioni 495 hadi kufikia bilioni 1.4 na kwa mwaka huu 2017/2018 imeongezwa na kufikia bilioni 2.02.

Hata hivyo alisema upatikanaji wa dawa huo utaongezeka kutokana na kwamba hivi sasa serikali kupitia bohari ya dawa(MSD) inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa ndani tofauti na zamani ambapo walikua wakinunua toka kwa mawakala

Waziri Ummy aliwapongeza Mkoa huo licha ya changamoto zote zinazowakabili katika vituo vya kutolea huduma bado mkoa huo unasonga mbele katika kukabiliana na tatizo la vifo vitokanavyo na na uzazi kwa vifo 117 kati ya vizazi hai laki moja wakati takwimu za kitaifa ni vifo 506

Kwa upande wa vifo vya watoto chini ya miaka mitano wamepunguza  na kuwa na vifo 31 kati ya vizazi hai laki moja ambapo takwimu za kitaifa ni 67,aidha kwa akina mama wajawazito wanaoenda kujifungulia kwenye vituo vya afya mkoa wa Rukwa ni akina mama 65 kati ya mia moja ambapo takwimu za kitaifa ni akina mama 64,?hapa niwapongeze mmepiga hatua sana?

Kutokana na jitihada za serikali za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano hivi karibuni ilinunua na kusambaza kwenye halmashauri zote vitanda ishirini na tano ikiwemo vitanda vitano kwa ajili ya kujifungulia pamoja na mshuka hamsini


Awali Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe.Justine Haule  aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitanda pamoja na mashuka na hivyo kupunguza changamoto ya vitanda katika wodi za akina mama wanaojifungua na alitaka changamoto kubwa ni kwamba mji wa rukwa unaendelea kukua hivyo bado huduma za afya zinahitajika sana ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages