Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo na team ya tanroad wafanya ukaguzi eneo la mradi interchange ubungo - Mtazamo News: Home
advertise here +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

TANGAZO


Tuesday, August 29, 2017

Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo na team ya tanroad wafanya ukaguzi eneo la mradi interchange ubungo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg.John L.Kayombo kwa kushirikiana na  Team kutoka TANROAD na  mkandarasi wa ujenzi  wa Ubungo Interchange  wamefanya ziara katika eneo la Mradi wa ujenzi wa Interchange kwa  lengo  la  kukagua  eneo la Mradi ambalo lina vibanda na wafanyabiashara ambao watalazimika kuondolewa ilo kupisha ukamilishaji wa mradi huo .


Mradi wa Interchange kwa Manispaa ya Ubungo ulizinduliwa Rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli tarehe 20/3/2017 ikiwa ni moja ya juhudi ya serikali katika kuboresha miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji na kuchochea mapinduzi ya viwanda  utakaopelekea   ukuaji wa uchumi ,pia kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa la kisasa zaidi.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano -UMC
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages