Header Ads


Makamu wa Rais Ahimiza Bima ya Afya kwa Wakazi wa Kizimkazi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi  kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati  wa Sherehe ya  Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.

Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.

Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.

Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.

Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja  na kuleta mshikamano katika jamii.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wakazi wa Kizimkazi Mkunguni wakati alipowasili tayari kujionea shughuli za ujenzi wa ukumbi wa Skuli ya Kizimkazi Sekondari
 Viongozi na wageni waalikwa wakijumuika kula chakula cha asili wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika Kizimkazi, mkoa wa Kusini Unguja.
  Wakina Mama wakishindana kusokota kamba ikiwa sehemu ya michezo inayochezwa siku ya sherehe za Siku ya  Wakizimkazi inayofanyika mwezi Agosti kila mwaka
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Post a Comment
Powered by Blogger.