Koka -Achangia Mil.3 Ujenzi wa Mradi wa Wanawake KKKT Tumbi - Mtazamo News: Home
advertise here +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

TANGAZO


Monday, August 14, 2017

Koka -Achangia Mil.3 Ujenzi wa Mradi wa Wanawake KKKT Tumbi

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka  amesali kanisa la KKKT Tumbi ambapo pamoja na mambo mengine amechangia 3,000,000/- kwenye ujenzi wa  mradi wa wanawake wa KKKT kanisani hapo.

Aliwataka wanawake ,vijana kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi .

Mapema akitoa salamu za waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ambaye alitakiwa awe Mgeni Rasmi katika siku hii lakini hakufika kwa sababu ya majukumu mengine, Mbunge Koka aliwasilisha 6,000,000/- mchango wa mhe  waziri  kwenye miradi hiyo ya akinamama wa KKKT .
 Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka ,mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja baada ya misa kwenye kanisa la KKKT Tumbi Kibaha.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages