Klabu ya Simba Yatembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 7 August 2017

Klabu ya Simba Yatembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba na mtoto  Mwamvita Hassan ambaye timu hiyo imemlipia shilingi milioni mbili kwa ajili ya gharama za upasuaji wa Moyo.
 Wachezaji wa timu ya Simba Haruna Niyonzima na Nicholaus Gyan walimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alipokuwa aliwaeleza madhara yatokanayo na magonjwa ya Moyo anayoweza kuyapata mchezaji awapo uwanjani. Baadhi ya viongozi wa timu hiyo pamoja na wachezaji walitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma wanazozitoa pamoja na kukabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mwamvita Hassan.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza umuhimu  wa mchezaji kupima magonjwa ya moyo ili kuepuka  kupata madhara ya ugonjwa huo wawapo uwanjani kwa baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo.
 Nahodha wa timu ya Simba Method Mwanjali akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo za mtoto Mwamvita Hassan (wa pili kulia) ambaye anatibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na mchezaji wa Timu ya Simba Haruna Niyonzima mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Simba Dkt. Anord Kashembe.
 Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau akiwaeleza wachezaji wa timu ya Simba aina mbalimbali za upasuaji wa moyo kwa watoto wanazozifanya wakati baadhi ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi  walipotembelea Taasisi hiyo leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi pamoja na wachezaji wa timu ya Simba mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages