Header Ads


Katibu Mkuu Sihaba Nkinga Ashiriki Kazi ya Ujenzi wa Zahanati ya Ufyemba Kata ya Wasa Mkoani Iringa

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa katika jitihda za kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa kushirikiujenzia wa  zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma za afaya kijijini. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinda akishirikiana na wakazi wa Kijiji cha ufyemba kubeba matofali katika kufanikisha ujenzi wa Zahanati kijiji cha Ufyemba kata ay wasa, iliyoko wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
 Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakishiriki katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya. 

 Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakimsikilizakwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati akiwahamasisha kujitolea katika kuibua, kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo katika Kijiji chao.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius Lunyungu ili kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi pesa kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Roganius Lunyungu zilizopatikana katika harambee  ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ufyemba wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kushiki kwa vitendo kazi za miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na kutekelezwa kwa kutumia nguvu za wananachi wenyewe katika kijiji hicho.


Picha na Erasto Chin’goro WAMJW IRINGA

No comments

Powered by Blogger.