MANISPAA YA UBUNGO YAZINDUA MAGARI MATANO 5 Pick up - HILUX - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 15 August 2017

MANISPAA YA UBUNGO YAZINDUA MAGARI MATANO 5 Pick up - HILUX

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John L.Kayombo (kushoto) akikata utepe kuzindua magari matano mapya,katikati ni Afisa utumishi mkuu wa Manispaa Ndg.Ally J Ally na pembeni Mweka Hazina wa Manispaa Ndg.Jane Machicho.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John L.Kayombo akiwasha moja kati ya gari jipya mara baada ya kuzindua
Muonekano wa magari mapya yaliozinduliwa na mkurugenzi wa manispaa ya ubungo John L.Kayombo 

Leo Jumanne August 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Mkurugenzi Ndg. John Lipesi Kayombo imezindua magari matano mapya Aina ya Pick- up  Hilux waliyoyanunua kwa fedha za mapato ya ndani ( OWN SOURCE)

Ikiwa ni moja ya mikakati ya awali ya Manispaa hii katika kuboresha mapato ya ndani yatakayoleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya kijamii kama Hospitali, zahanati, shule na Ujenzi wa vituo vya afya magari hayo yote yamepelekwa katika idara ya Fedha na biashara kitengo Cha Mapato.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. John Lipesi Kayombo alisema ununuaji wa magari hayo ni kwa ajili ya kuboresha zaidi ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kuzipeleka Gari hizo kwa wakusanyaji wa mapato moja kwa moja ambao wako kwenye kata na mitaa ndani ya Manispaa ya ubungo

"Manispaa ya Ubungo tulikuwa na magari machache sana, ukusanyaji wa mapato ulikuwa ni mzuri  lakini tumeona bora tuongeze vitendea kazi ili kufikia lengo letu la kukusanya zaidi shillingi billioni 23 ambayo ndio Bajeti ya 2017/18  ili kutekeleza miradi  ya maendeleo kwa asilimia 100 na kuweza kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi" alisema Kayombo.

Pia Mkurugenzi Kayombo aliwashukuru Madiwani sambamba na watumishi wa Manispaa hiyo kwa ushiriki wao na hatimaye kuweza kuongeza mapato ya Manispaa hiyo.

Akizungumza baada ya uzinduzi na kukabidhiwa magari hayo  kwa niaba ya Idara ya fedha mwaka hazina wa Manispaa ya Ubungo Ndg.  Jane Machicho alimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na menejimenti nzima kwa kutatua changamoto ya usafiri katika ukusanyaji wa mapato kwani itasaidia kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo na hatimaye kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato la shilingi billioni 23 kwa mwaka.

Manispaa ya Ubungo tangu kuanzishwa kwake ambapo ni takribani miezi tisa sasa imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuboresha mapato ya manispaa ambapo moja wapo ilikuwa ni kutatua tatizo la usafiri katika ukusanyaji wa mapato katika kata za wilaya ya Ubungo.

Hongera Baraza la Madiwani, Mkurugenzi na menejimenti nzima ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

#UBUNGO YA TOFAUTI

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO-UMC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages