Floyd Mayweather Aweka Rekodi Mpya ya Dunia.... Amtoa Kamasi McGregor - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 27 August 2017

Floyd Mayweather Aweka Rekodi Mpya ya Dunia.... Amtoa Kamasi McGregor

Bondia Floyd Mayweather ameweka rekodi katika ulimwengu wa ngumi baada ya kushuka ulingoni mara 50 bila kupoteza hata pambano mara moja.

Rekodi hiyo mpya ameiweka leo (Agosti 26 kwa saa za Marekani) baada ya kumdhibiti Conor McGregor ambaye alikuwa ni hasimu wake katika pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu katika mzunguko wa 10 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa alama 87 dhidi ya 84 za Conor.

McGregor alianza vizuri pambano hilo kwa kumtwanga Mayweather lakini baadae kibao kilimgeukia huku akitupiwa makonde na kushindwa kujibu.

Baada ya pambano hilo lililofanyika katika uwanja uliopo Las Vegas, Mayweather amesema kuwa Conor ni mpiganaji mzuri kuliko alivyodhania lakini ameweza kuwapa mashabiki wake na wapenzi wa ngumi, kile walichokuwa wakikisubiria kwa hamu.

Mayweather amesema kuwa hilo lilikuwa ni pambano lake la mwisho na ana uhakika kwamba alichagua mshindani mzuri (Conor) ambaye alimpa ushindani mkubwa.

Hapa chini ni baadhi ya picha kutoka kwenye pambano hilo;

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages