Epukeni dawa za kulevya-Waziri Stella Manyanya - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 31 August 2017

Epukeni dawa za kulevya-Waziri Stella Manyanya

 Na Tiganya Vincent RS-TABORA

SERIKALI imewaonya wanafunzi kuepuka matumizi ya dawa za kulevya ambayo ndio wakati  mwingine yawasababisha kujiingiza vya uhalifu na vurugu ambazo hatimaye zinawasababisha baadhi yao kusimamishwa masomo na kukatiza ndoto zao.

Agizo limetolewa jana wilayani Tabora na  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya  wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Tabora ili kujionea maendeleo ya ukarabati chini ya utaratibu wa ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini.

Aliwaambia kuwa wanafunzi wote nchini wanatakiwa kufuata Sheria za Shule na za Nchi ili kuhakikisha anamaliza masomo yake bila kupata matatizo ikiwemo kufikishwa mahakamani.

“Unatakiwa kufuata Sheria na taratibu za shule kama ulivyoelekeza , ukitoroka shule na kwenda mitaani ukileta fujo …ukileta vurugu utashughulikiwa kama ulivyokutwa huko huko…kwa sababu mwanafunzi anatakiwa kuwa eneo la shule sawa “ alisisitiza Naibu Waziri huyo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwataka Wanafunzi wa Shule za Wasichana ya Tabora kuepuka kujiingiza katika vitendo vitakavyokatisha ndoto zao kwa sababu ya kupata ujauzito.

Alisema kuwa vema kwa wakasoma kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kukatisha ndoto zao kwani jamii na taifa linawategemea sana kuja kushika nafasi mbalimbali.

Naibu Waziri huyo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wawe tayari kukabiliana na ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Aidha Manyanya aliwataka walimu wanaofundisha shule za watoto wenye vipaji maalumu kuhakikisha wanajituma kwa bidii katika kuwafundishi wanafunzi hao ili waendelee kufanya vizuri kama walivyotoka shule za awali.

Alisema kuwa itasikitisha sana kuona mtoto aliingia katika shule hiyo kwa ajili ya kipaji chake maalumu na inapifika mitahani yake anashindwa au anafanya vibaya kinyume na ilivyokuwa hapa awali.

Akitoa taarifa ya ukarabati unaoendelea Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Marwa Robert alisema kuwa hadi hivi sasa kazi mbalimbali ukarabati unaendelea vizuri na zimebaki siku 60 ili mjenzi akabidhi kazi.

Alisema kuwa ukarabati huo utagharimu shilingi milioni 999 ambapo hadi hivi sasa kazi zilizokwishafanyika ni pamoja na kubomoa na kuziba nyufa, kupaka rangi, ukarabati wa madirisha , milango, kurejesha vyoo, ukarabati wa maktaba ya zamani, ujenzi wa maktaba mpya na kuandaa miundo mbinu ya maji.

Hivi karibuni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Milambo walitoroka shuleni usiku na kuvamia sherehe za mkazi wa Tabora  na kusababisha hasara kubwa na kujeruhi baadhi ya watu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages