WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPOKEA MISAADA YA UHIFADHI KUPAMBANA NA UJANGILI - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Thursday, 6 July 2017

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPOKEA MISAADA YA UHIFADHI KUPAMBANA NA UJANGILI

Na Twaha Twaibu (Afisa Habari na Mawasiliano-TAWA)

Makala hii inafuatia ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej.Gen. Gaudence S. milanzi  aliyofanya hivi karibuni katika kutembelea Mapori ya Akiba ya Lukwa-Piti katika Mkoa wa Mbeya, akifuatana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. Martin loibooki. Dhumuni kubwa la ziara hiyo ilikuwa kwenda kupokea vifaa vya doria ,magari na kukabidhiwa ofisi ya pori la Pitikwa msaada ambao ulitolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la uhifadhi liitwalo ‘Wildlife Conservation Society- WCS’ Makao Makuu yake yako Iringa ila linafanya kazi kwa kushirikiana na uongozi wa Pori la Akiba Lukwati-piti
TAASISI YA KIMATAIFA YA KIJAMII YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI YA ‘WILDLIFE CONSERVATION SOCIETY-WCS ) IMETOA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 940 AMBAZO ZIMETUMIKA KUJENGA OFISI, KUNUNUA VITENDEA KAZI YAKIWEMO MAGARI NA KUGHAMARAMIA MAFUNZO KWA ASKARI WA WANYAMAPORI WA MAPORI YA AKIBA YA LUKWATI- PITI ILI KUKABILIANA NA UJANGILI NA UWINDAJI HARAMU AMBAO UMESABABISHA VIFO VYA TEMBO WAPATAO 23 TANGU MWAKA 2013 MPAKA SASA. UJENZI WA JENGO LA OFISI NA MAGARI VILIKABIDHIWA KWA MEJ.JENERALI GAUDENCE S. MILANZI ( KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII). VILEVILE SHIRIKA LA WCS WAMETOA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJANGILI PICHA ITAKAYOFUATA NI BAADHI YA ASKARI WANYAMAPORI WALIYOSHIRIKI KATIKA MAFUNZO WAKIONGEA NA KATIBU MKUU
  KATIBU MKUU  (MWENYE KOTI NYEUSI) AKIKATA UTEPE WA UZINDUZI WA OFISI YA PORI LA PITI KULIA KWAKE NI KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TAWA BW.MARTIN LOIBOOKI NA KUSHOTO NIMENEJA WA PORI LA RUKWA/PITI BW.AMBROSE MUNGO’NG’O.

AKIONGEA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI MIRADI HIYO IKIWEMO JENGO LA KISASA, MAGARI NA VIFAA VYA DORIA KWA SERIKALI YA TANZANIA, MKURUGENZI WA TAASISI YA KIJAMII YA KIMATAIFA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI IITWAYO WORLD CONCERVATION SOCIETY, AARON NICHOLAUS AMESEMA WCS INAJIVUNIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUIMARISHA UHIFADHI NA AMEZUNGUMZIA UMUHIMU WA MAPITO YA WANYAMAPORI AMBAYO YAMEATHIRIWA NA SHUGHULI ZA BINADAMU LICHA YA UMUHIMU WAKE KWA UHIFADHI AMBAPO KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AMESEMA MSIMAMO WA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA UHIFADHI UKO WAZI KWANI MALIASILI HIZO ZINA UMUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA
 BW.MARTIN LOIBOOKI (KAIMU MKURUGENZI MKUU-TAWA) AKITOA TAARIFA FUPI YA MAPORI YA AKIBA RUKWA/PITI MBELE YA KATIBU MKUU.

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA WANYAMAPORI TANZANIA TAWA, MARTIN LOIBOOKI AMESEMA TAWA INATAMBUA WAJIBU WAKE NA MALENGO YA KUANZISHWA KWA MAMLAKA HIYO YA KUSAIDIA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JAMII NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI KUPITIA SEKTA YA WANYAMAPORI NA AMEISHUKURU WCS KWA KUWA MFADHILI WA KWANZA KUFADHILI SHUGHULI ZA UHIFADHI KATIKA MAPORI YA LUKWATI- PITI
 BAADHI YA KIKOSI CHA ASKARI KILICHOHUDHURIA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJANGILI (RAPID RESPONSE TEAM)
 KATIBU MKUU AKIONGEA NA BAADHI YA KIKOSI CHA ASKARI WALIYOPATA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJANGILI 
 KATIBU MKUU AKIWA NA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA TAWA PAMOJA NA WCS MBELE YA JENGO JIPTA LA PORI AKIBA PITI.
 KATIBU MKUU (WA TATU KUTOKA KUSHOTO) AKIWA AMEPANDA KWENYE MWINUKO (OBSERVATION POINT) NDANI YA PORI LA AKIBA LUKWATI  AKIANGALIA MADHARI YA PORI HILO KARIBU NA ZIWA RUKWA
 BAADA YA DORIA YA PORI LA AKIBA LIKWATI-PITI  KATIBU MKUU AMEPUMZIKA NA KUPATA MAJI AKIFUATANA NA BW.MARTIN LOIBOOKI KATIKA ENEO LA (OBSERVATION POINT) NDANI YA PORI LA HILO.
KATIBU MKUU (KULIA) KATIKA SAFARI HIYO ALIFUATANA NA WANDISHI WA HABARI WA KUTANGAZA PORI LA AKIBA LUKWA LUKWATI/PITI. ANAONGEA NA MWANDISHI WA HABARI BW. VEDASTO MSUNGU KUTOKA ITV NDANI YA KAMBI YA UWINDAJI WA KITALII KATIKA PORI HILO.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337