MALIPO YA KODI YA PANGO LA ARDHI YAENDELEA KWA KASI NCHINI - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 2 July 2017

MALIPO YA KODI YA PANGO LA ARDHI YAENDELEA KWA KASI NCHINI

Wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiwa imetoa ongezeko la siku 15 kwa wadaiwa wa Kodi ya Pango la Ardhi kuendelea kufanya malipo hayo; Vituo mbalimbali vya Makusanyo hayo vimeonekana kufurika.
Katika picha ni Maeneo kadhaa tu nchini, ambapo Wananchi wameendelea kujitokeza kufanya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi.
 Kituo cha Makusanyo- Kivukoni, Magogoni (Dar es Salaam)
Hatahivyo, Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi yameboreshwa hivi karibuni kwa Mfumo Mpya wa Kielektroniki ambapo mdaiwa ana uwezo wa kufanya malipo hayo kwa njia ya simu ya Mkononi au kwa kuingia; (http://landrent.lands.go.tz/landrent).
Aidha, tathimini imeonyesha kuwa baadhi ya Wananchi wameshafanikiwa kufanya malipo haya kwa kutumia Mfumo huu Mpya wa Kielektroniki.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages