WATOTO WENYE MATATIZO YA USIKIVU SASA KUTIBIWA NCHINI. - Mtazamo News
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Wednesday, 7 June 2017

WATOTO WENYE MATATIZO YA USIKIVU SASA KUTIBIWA NCHINI.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Muhimbili Prof.Charles Majinge.

Picha Na Ally Daud-WAMJW Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kushoto akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam katikati ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Muhimbili Prof.Charles Majinge.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya  na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimsalimia mlezi Theodora Myalla aliyembeba mtoto  Meckzedeck Kibona (2) mkazi wa Tegeta aliyepandikizwa kifaa cha usikivu wakati alipozindua huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya watoto waliopandikizwa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
....
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

 WATOTO wenye matatizo ya usikivu watapata matibabu  ya kupandikizwa vifaa vya usikivu hapa nchini katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili badala ya kwenda nje ya nchi kwa matibabu kama ilivyokuwa awali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipozindua huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.

“Serikali haitapeleka mgonjwa mwenye matatizo ya kusikia nje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa vifaa vya kusikia na badala yake atatibiwa nchini ili kupunguza rufaa za wagonjwa wan je ya nchi” alisema Mh. Ummy.

Aidha Waziri Ummy  amesisitiza juu ya umuhimu wakujiunga na mfuko wa Afya wa Jamii wa NHIF ili kupata fursa ya kutibiwa kwa gharama ndogo zaidi, huku akisisitiza kuwa wananchi wote watakaokuwa na kadi ya NHIF wataweza kupata matibabu ya upandikizaji wa kifaa cha kusikia bure kupata huduma hii.

 Mbali na hayo Mh. Ummy  ameahidi kuwa Serikali kupitia Wizara yake ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuunga mkono kwa kuisaidia hospitali ya Muhimbili ili kuendelea kufanikisha upasuaji wa Watoto hivyo kupunguza gharama inayopata Serikali kusafirisha Watoto hao nje ya nchi pindi wapatapo matatizo hayo.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Lawlence Mseru amsisitiza kuwa moja kati ya  mipango  ya Hospitali ya Muhimbili ni kuhakikisha kuwa wanapunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi kila mara jambo linaloigharimu Serikali pesa nyingi.

Aidha Dkt. Mseru aliongeza kuwa licha ya kufanikisha tukio hilo la Kihistoria  wanaomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kusaidia kuboresha Wodi za Wagonjwa mahututi, ununuzi wa Vifaa tiba, kuongeza vyumba vya upasuaji jambo litalopunguza msongamano  wa shughuli za hospitali pia kuongeza Wataalamu waendao nje ya nchi kwaajili ya mafunzo ili kuendeleza huduma katika nchi yetu jambo litakalosaidia kuwa na Wataalamu wengi hivyo kuweza kufanikisha huduma kwa wagonjwa wengi zaidi.
Nae  Prof. Sunil Narayan Dutt kutoka Hospitali ya Apollo  nchini India ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada inayoonesha hasa katika kutetea haki za watoto.

Kwa upande Bi. Hilda Bohela ambae ni mzazi wa Apulie Bohela aliyepata huduma hiyo nchini  amewasihi wazazi wenzie kuwapeleka watoto kufanyiwa uchunguzi pindi waonapo hali isiyokuwa yakawaida kwa watoto wao na kuachana na mila potofu jambo linalopelekea watoto wengi kupata ulemavu .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages