WATOTO WA KIKE WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOFANYA WASIFIKIE MALENGO - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Breaking

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222

Post Top Ad

Post Top Ad


Sunday, 25 June 2017

WATOTO WA KIKE WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOFANYA WASIFIKIE MALENGO

 Meneja wa Bima ya Maisha wa NIC , Isihaka Kibamba akimkabidhi sehemu ya msaada wa chakula,Mama Mlezi  wa Kituo cha Eco Village ,Arafa Someya kilichotolewa na wafanyakazi wa NIC kwa kushirikiana na mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega leo  na , kushuhudiwa  na viongozi wa kituo na watendaji wa NIC.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Mwakilishi wa Mbunge wa Mkuranga, Omary Kisatu(wa kwanza kulia) akitoa shukurani kwa msaada uliotolewa na NIC kwa kushirikiana na Mbunge huyo kwa kuona umhimu wa kutoa msaada katika kituo cha Eco Village kilichopo Vikindu Kisemvule leo.
Watendaji wa NIC , Viongozi wa Kituo cha Eco Village wakiwa katika picha ya pamoja  na Watoto wa kituo hicho leo .

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Watoto wa Kike ni moja kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa ukaribu kutokana na changamoto mbalimbali zinazofanya wasiweze kufikia ndoto zao .

Hayo ameyasema leo Meneja wa Kituo cha Kulelea Watoto na Yatima na wanaoishi katika Mazingira  Magumu wa Kituo cha Eco Village , Said Ngalula wakati wa kupokea msaada wa vyakula vilivyotolewa na Shirika la Taifa la Bima (NIC) kwa kushirikiana na Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega.

Ngalula amesema kituo hicho kina watoto 20 wa kike ambao wamewachukua katika maeneo mbalimbali kwa ajili yakuweza kuwaendeleza kielimu na kuweza kuona wamekombolewa.

Amesema wanatarajia kuongeza watoto wa kiume ili nao waweze kupata elimu katika kituo hicho kwa kusomeshwa katika shule za msingi pamoja na Sekondari.

Nae Meneja wa Bima ya Maisha wa NIC , Isihaka Kibamba amesema wafanyakazi wameweza kuchangishana na kuweza kupatikana kwa vyakula hivyo.

Kibamba amesema japo kitu walichotoa ni kidogo lakini inaonyesha kuguswa kwao katika mahitaji yaliyopo sasa pamoja nakufurhi katika siku kuu ya Idd el Fitri.

No comments:

Post Top Ad

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222