TBL GROUP YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA MAFUNZO WANAFUNZI. - Mtazamo News
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 17 June 2017

TBL GROUP YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA MAFUNZO WANAFUNZI.

 Meneja wa mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga, akiongea na  wanafunzi.
 Afisa wa Masuala Endelevu ,Irene Mutiganzi akiongea na wanafunzi.
 Afisa Mawasiliano ,Abigail Mutaboyerwa,akisisitiza jambo kwa wanafunzi. 
 Wanafunzi wakimsikiza kwa makini Afisa Mawasiliano kutoka TBL Group,Amanda Walter.
Wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya Oysterbay wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group,baada ya mafunzo ya kuchambua changamoto za maisha wakati wa maadhimisho ya siku ya motto wa Afrika.

Katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwishoni mwa mwiki baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group walijitoa kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akiongelea maadhimisho hayo,Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,alisema kuwa siku hii ni muhimu kwa kampuni kwa kuwa kupitia sera yake ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ imelenga kuhakikisha  inashiriki ipasavyo kuhakikisha inachangia kukabiliana na changamoto za kijamii kwenye maeneo inayofanyia biashara lengo kubwa likiwa ni kuifanya dunia iwe sehemu bora ya kuishi.

“Sera yetu ya  Kujenga Dunia Maridhawa hailengi katika suala la mazigira  na maji pekee bali pia kujenga jamii imara na ndio maana  tunalipa suala la elimu kipaumbelee kikubwa na  leo  tumetembelea shule ya msingi Oysterbay, moja ya shule iliyopo maeneo yetu ya biashara kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi elimu ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye safari yao ya kielimu na kutimiza malengo na ndoto zao”.Alisema Tenga.

Alisema baadhi ya maofisa wa TBL Group walipata fursa ya kuongea na wanafunzi wa darasa la sita  wa shule hiyo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto  za maisha na umuhimu za kuzingatia masomo yao ili waweze kutimiza ndoto zao za baadaye katika maisha yao ya baadaye wakiwa ni watoto wa kiafrika.

Tenga alisema mbali na kuwapatia mafunzo kampuni imezindua shindano la wiki moja la kuandika insha ya maneno 300 kwa wanafunzi  hao kuhusiana na changamoto zilizopo katika safari yao ya kielimu na jinsi ya kuzikabili ambapo wanafunzi watatu wataoshinda watapata zawadi kutoka TBL .

Alisema mpango huu wa kukutana na wanafunzi na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo ni mpango endelevu ambao utaendelea kutekelezwa na wafanyakazi wa kampuni wenye taaluma mbalimbali katika maeneo yote  ambako inaendeshea biashara zake nchini pote.

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages