SOCIAL ACTION TRUST FUND (SATF) YAICHANGIA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) SHILINGI MILIONI 10 KWA AJILI YA GHARAMA ZA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO WATANO - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 16 June 2017

SOCIAL ACTION TRUST FUND (SATF) YAICHANGIA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) SHILINGI MILIONI 10 KWA AJILI YA GHARAMA ZA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO WATANO

 Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue  akimkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za  upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  akimshukuru Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue  mara baada ya kumkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za  upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
 Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue  akimsalimia mtoto Goodluck Msele ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na hali yake inaendelea vizuri. SATF imechangia shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za  upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau (katikati) akimwelezea Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue  (kushoto) kuhusu aina mbalimbali za magonjwa ya moyo yanayowasumbua watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msimamizi wa Wodi ya watoto Afisa Muuguzi Rogers Kibula.
Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue  akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau wakati akimuelezea jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika katika Taasisi hiyo.

Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages