SIKU YA MAZINGIRA KISHAPU - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 6 June 2017

SIKU YA MAZINGIRA KISHAPU

Mgeni rasmi wa Siku ya Mazingira, Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack kwenye kilele cha Siku ya Mazingira kimkoa wilayani humo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akipeana mkono na mwenyekiti, Boniface Butondo baada ya kupokea cheti kwa ajili halmashauri yake kufanya vizuri katika upandaji miti.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo akizungumza wakati wa sherehe hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia alizeti kwenye banda la Halmashauri ya wilaya hiyo wakati wa sherehe hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiwa na viongozi wengine wakimsikiliza mtalaamu kuhusu majiko yasiyotumia kuni wakati akitembelea mabanda.
Ofisa Kilimo kata ya Ngofila, Genes Tarimo (kushoto) akiwapa maelezo kuhusu madumu maalumu vya kuchemshia maji ya kunywa mgeni rasmi na viongozi aliombatana nao.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josphine Matiro (kushoto) wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi (katikati).
Ofisa kutoka Mgodi wa Williamson Mwadui akitoa maelezo kwa wageni kuhusu jiko linalotumia sola kupikia vyakula mbalimbali bila kutumia kuni wala mkaa.
Sehemu ya vitalu vya miche vikiwa katika banda la maonesho vikiwa tayari kwa ajili ya kuonesha wananchi namna ya kupandwa.
Wananchi wakitembelea banda la halamashauri ya wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (wa pili kushoto) akionesha furaha yake kwa kuserebuka na kwaya ya wanafunzi.
Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akipata maelezo kutoka banda la mgodi wa Williamson Mwadui. Nyuma yake ni mkurugenzi mtendajihalmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametumia Siku ya Mazingira Duniani kuwaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya ukataji miti.

Ametoa agizo hilo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba leo wakati wa kilele cha siku hoyo kilichofanyika kimkoa kata ya Mwamashele wilayani hapa.

Alisema kuwa wananchi wengi hawaelewi kuwa tunapokata miti kwa wingi tunatishia uhai wetu na wa wanyama hali inayotokana na ukosefu wa mvua na hivyo kusababisha ukame.

Telack alisema kuwa misitu ndiyo mhimili mkubwa wa kulinda mazingira yetu na kutupatia nishati, dawa za asili, vifaa vya ujenzi pamoja na kuboresha hali ya hewa.
“Pamoja na muhimu wa misitu kwa binadamu na mazingira imekumbwa na uharibifu mkubwa katika mkoa wetu wa Shinyanga kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya uchomaji mkaa,” alisema.

Aliongeza kuwa uchomaji wa mkaa katika maeneo mengi kama vile Nyasamba umekuwa kama shughuli ya kujipatia kipato na hivyo kutishia kutoweka kwa misitu.
Aliwataka wadau kutumia nishati mbadala kama vile vinyeshi vya wanyama na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi hayo kwani matumizi ya mkaa ni adui wa mazingira.

Mkuu huyo wa mkoa alionya kuwa uchomaji mkaa na utumiaji wake huongeza hewa ya ukaa na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi na hatimaye kuleta ukame.
“Hivyo ni vema wananchi tubadilike na tuachane na matumizi ya rasilimali zetu kuwa endelevu kwa kupanda miti zaidi ili tuhifadhi ardhi, vyanzo vya maji na kuboresha hali ya hewa,” alisema.

Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, wakurugenzi wa halmashauri za Ushetu, Msalala, Shinyanga na Kahama.

Sherehe hizo ambazo kitaifa zilifanyika jana mkoani Mara zinachagizwa na kaulimbiu ya Hifadhi ya Mazingira ni muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages