RC TABORA TOENI ELIMU SAHIHI YA MATUMIZI YA VYANDARUA - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 6 June 2017

RC TABORA TOENI ELIMU SAHIHI YA MATUMIZI YA VYANDARUA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akifungua Mkutano jana mjini Tabora wa viongozi mbalimbali kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo.

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na wakuu wa Idara za halmashauri zote za mkoa huo kutoa elimu ya usafi wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu  ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
 
Bw. Mwanri alitoa wito huo jana mjini Tabora  wakati akifungua mkutano wa siku moja   kwa viongozi mbalimbali mkoani humo kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolewa huduma za afya na shule za msingi.

Alisema kuwa elimu sahihi itasaidia wananchi kuacha kutumia vyandarua kwa matumizi mengine badala ya kujikinga na mbu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa na malaria .

Mkuu huyo Mkoa aliongeza wananchi wakifahamu juu ya usafi wa mazingira utasaidia kuondoa mazalia mbu katika makazi yao.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito kwa watalaam kusaidia mkakati wa kuangamiza kabisa mazalia ya mbu kama sehemu ya kuondoa ugonjwa wa malaria hapa nchini.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora aliiomba jamii kubadirika na kuanza kutumia vyandarua vyenye viutilifu ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
 
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema mpango wa kugawa vya ndarua katika vituo vya kutoa huduma za afya ,shule za msingi na katika ngazi ya familia unakusudia kupunguza maambuzi ya maralia hapa nchini.
 
Aliongeza kuwa vyandarua hivyo vitasaidia kupunguza  maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani hapa kutoka asilimia 19.5 ya sasa na kushuka zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages