OKWI KUZIBA PENGO LA AJIBU - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 16 June 2017

OKWI KUZIBA PENGO LA AJIBU

Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao.

ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. 

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi.


Tayari mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa timu ya Simba Zacharia Hans Poppe ametua nchini Uganda kunamalizana na mchezaji huyu ambaye anacheza timu ya AS Villa

Updates: Muda mfupi uliopita, klabu ya Simba kupitia msemaji wao Haji Manara wamethibitsha Okwi amemwaga wino wa kuitumikia Simba, mkatabawa miaka miwili. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages