MKUU WA MKOA AWAPONGEZA MBEYA PRESS CLUB KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA - Mtazamo News: Home
advertise here +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

TANGAZO

advertise here +255755 300 337

Friday, June 30, 2017

MKUU WA MKOA AWAPONGEZA MBEYA PRESS CLUB KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

Akabidhi kadi za bima za Afya kwa wanachama wa Mbeya press club na kuwapongeza kwa uamuzi wa kujiunga na BIMA YA Afya

Asema kila binadamu ni mgonjwa mtarajiwa hivyo uamuzi wa kujiunga na bima ni uamuzi mzuri kwani hakuna binadamu anayejua siku YA kuumwa na kwa waandishi wanafanya kazi ktk mazingira magumu hivyo kuwa na bima YA afya ni jambo muhimu
Amewataka  na kuwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia bima waandishi wao wa habari

Amewaomba waandishi wa habari kuandika habari za kuwahamasisha wananchi kujiunga na bima YA Afya

Ktk hafla hiyo Mbeya press club wamempongeza Rais Dr John Magufuli kwa kazi nzuri za kuwatetea wanyonge , kulinda na kutetea raslimali za nchi

Mkuu wa Mkoa amepokea shukrani hizo na kuhaidi kuziwasilisha kwa mheshimiwa Rais na kuwaomba Mbeya Press club kuendelea  kumuunga mkono mheshimiwa Rais na kuyaandika yote mazuri anayoyafanya Rais  na serikali yake

Post Bottom Ad


Pages