MKUU WA MKOA ATEMBELEA BONDE LA IHEFU WILAYA YA MBARALI - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 29 June 2017

MKUU WA MKOA ATEMBELEA BONDE LA IHEFU WILAYA YA MBARALI

Ni eneo OEVU na CHANZO cha maji mto Ruaha Mkuu

 Aupongeza uongozi wa wilaya na wananchi kwa kuitikia maelekezo YA serikali YA mkoa kuhusu kulinda eneo hilo na amefurahi Kukuta eneo hilo lipo salama  hakuna mifugo,uoto wa asili umeanza kurejea na Maji kutiririka vizuri mto Ruaha

 Amewaonya wananchi wachache wanaopeleka mifugo nyakati za usiku na kuzitoa alfajiri na ametangaza ulinzi na doria YA askari wa wanyama pori utafanyika masaa 24
Amewataka wananchi kutofanya shughuli eneo la Ihefu kwani eneo hilo ndiyo chanzo cha mto Ruaha kwa ajili ya kutiririsha Maji kupeleka Hifadhi YA Ruaha na bwawa la Mtera

 Amesema ili kutekeleza Agizo la Makamu wa Rais mhe Samia Suluhu la kurejesha EKOLOJIA YA mto Ruaha serikali YA Mkoa itasimamia sheria YA kulinda vyanzo vya Maji , kuondoa mifugo maeneo  oevu na hifadhi, kuweka alama mifugo ili kuzuia uingiaji mifugo kiholela ktk Mkoa wa Mbeya

Amewatoa hofu wananchi kutosikiliza propaganda za kuhamishwa badala yake waendelee na  shughuli zao za kujipatia kipato na maendeleo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages