MATUKIO KATIKA PICHA YA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA KUCHUNGUZA MAKINIKIA - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 13 June 2017

MATUKIO KATIKA PICHA YA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA KUCHUNGUZA MAKINIKIA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akielezea adidu za rejea walizokuwa wamepewa Kamati ya Pili ya Kuchunguza Makinikia wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti yao kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Wapili kutoka kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini Profesa Nehemia Ossoro  akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti yao leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
 Mwakilishi wa Wazee Joseph Butiku akitoa neon kwa niaba ya wazee wote wakati wa hafla ya kumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wapili kulia) ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ripoti ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia ripoti ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akipitia ripoti ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma.
 Wajumbe wa Kamati ya Pili iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuchunguza Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakiwa katika hafla ya kukabidhi ripoti yao leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Kamati hiyo inayoundwa na wajumbe nane wanataaluma za uchumi, Sheria na Takwimu.
 Baadhi ya waalikwa wakifuatilia hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya Wasanii wa Kundi la Tanzania Allstars wakifuatilia hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wasanii hao walialikwa maalum kutokana na wimbo wao unaohimiza uzalendo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Momose Cheyo walipokutana katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiteta jambo na Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Kilimanjaro, Amos Makalla na Anna Mghirwa walipokutana katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Merdard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa walipokutana katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati Maalum ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wasanii pamoja na wajumbe wa Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini na  mara baada ya hafla ya kukabidhiwa ripoti ya Kamati hiyo kumalizika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages