MANISPAA YA TABORA TENGENI ENEO LA MAHARUSI KUPANDA MITI-MWANRI. - Mtazamo News
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 5 June 2017

MANISPAA YA TABORA TENGENI ENEO LA MAHARUSI KUPANDA MITI-MWANRI.

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora umeagizwa kutenga maeneo (bustani) maalum kwa ajili Maharusi kutoka madhehebu mbalimbali waze kushiriki zoezi la  kupanda miti ili ukumbusho wa siku ya ndoa yao.
Agizo hilo limetolewa jana  na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yaliyofanyika katika Manispaa ya Tabora na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Hifadhi za Mazingira Muhili wa Tanzania ya Viwanda”.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia Maharusi kutoka madhehebu mbalimbali kuweka kumbumbuku ya kihistoria ambayo itakuwa faida kwao na kizazi chao.
Bw. Mwanri alisema kuwa Harusi itapendeza zaidi kama wanandoa mkoani humo watauma kuunga mkono zoezi linaloendelea la upandaji miti kwa kupinga picha wakipanda miti na kuwa tayari kuhakikisha inaendelea vizuri.
Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa maharusi hao baada ya kupanda miti na kuitunza wanaweza kuweka kumbukumbu ya majina yao ili kuonyesha mchango wao katika utunzaji wa mazingira siku walipoamua kuanza maisha mpya.
Aliongeza kuwa eneo hilo linaweza likapangiliwa vizuri kwa ajili kulifanya kuwa kivutio sio tu kwa wenyeji hata wageni na hivyo kuingizia Manispaa mapato kutokana tozo katika huduma nyingine kutoka kwa watalii.
Bw. Mwanri alisisitiza kuwa kumbukumbu nzuri kwa Bwana na Bibi ambayo wanayoweza kuipatia jamii inayowazunguka na kubaki katika historia ya maisha yao ni kuhakikisha kuwa siku ile ya ndoa wanapanda miti na kuitunza ili ije iwe hamasa kwa watoto wao watakaojaliwa na Mwenyezi Mungu.

Bw. Mwanri alisema kuwa siku ya ndoa baada ya kufunga pingu za maisha ni vema katika ratiba yao wakaweka na kipengelea cha kupanda miti kama ilivyo kwa wengine wanapomaliza shughuli ya ndoa watembelea vivutio mbalimbali kwa ajili ya picha za ukumbusho wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages