MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA: RUKWA - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 17 June 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA: RUKWA

 Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akijibu hoja mbalimbali za kiutumishi zilizojitokeza katika kikao hicho kilichofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais,UTUMISHI Bw. Mathew Kirama.
 Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais,UTUMISHI Bw. Mathew Kirama akitoa ufafanuzi wa masuala ya kinidhamu katika Utumishi wa Umma katika kikao kati ya viongozi waandamizi kutoka UTUMISHI na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa,Sumbawanga,Kalambo,Nkasi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga Bw. Deodatus Kangu akiuliza swali wakati wa kikao kati ya viongozi waandamizi kutoka UTUMISHI na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa,Sumbawanga,Kalambo,Nkasi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
 Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa Bw.Bernad Makali (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za kiutumishi wakati wa kikao kazi kilichofanyika ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa Bw.Aboubakar Kunenge akifuatilia kikao hicho.
 Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa,Sumbawanga,Kalambo,Nkasi wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba (hayupo pichani) akijibu hoja mbalimbali za kiutumishi zilizojitokeza katika kikao hicho ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma,kikao kilifanyika jana alfajiri.
Mkuu wa Idara ya Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi akichangia mada wakati wa kikao kati ya viongozi waandamizi kutoka UTUMISHI na Mviongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rukwa,Sumbawanga,Kalambo,Nkasi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages