KATIBU MKUU - UTUMISHI AHITIMISHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 KWA KUKUTANA NA WATENDAJI WA MKOA WA SIMIYU NA KUTEMBELA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MEATU - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Breaking

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222

Post Top Ad

Post Top Ad


Saturday, 24 June 2017

KATIBU MKUU - UTUMISHI AHITIMISHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 KWA KUKUTANA NA WATENDAJI WA MKOA WA SIMIYU NA KUTEMBELA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MEATU

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akipata maelezo ya usindikaji maziwa kutoka kwa Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Gerald Baruti alipotembelea Kiwanda cha kusindika Maziwa (Meatu Milk) kilichoanzishwa na vikundi vya vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiangalia bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, alipotembelea shughuli za maendeleo za Wilaya ya Meatu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Upendo Naftali
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (Wa tatu kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (Wa pili kulia) kabla ya kukutana na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony Mtaka (katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia), alipokuwa akizungumza nae kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.

No comments:

Post Top Ad

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222