HALOTEL YAJIVUNIA KUJIUNGA MFUMO WA ULIPAJI KODI KIELECTRONIKI - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 8 June 2017

HALOTEL YAJIVUNIA KUJIUNGA MFUMO WA ULIPAJI KODI KIELECTRONIKI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, Akizungumza na waandishi wa habari 
wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa pongezi kwa serikali kwa kuanzisha  
mfumo wa wawazi wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kampuni hiyo  
ni miongoni mwa makampuni matatu ya simu ya kwanza kujiunga na mfumo huo 
ambao amefafanua kuwa unaweka uwazi katika biashara. Pamoja nae katika 
picha ni Meneja Uhusiano wa Kampuniu hiyo Stela Pius na Meneja 
Mawasiliano Hindu Kanyamala (Kushoto).
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari, Wakati kampuni hiyo ilipofanya mkutano wa kuipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielectroniki. Katikati ni Mkurugenzi Mtenzaji wa Kampuni hiyo Le Van Dai na Meneja Uhusiano Stella Pius.


Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imeipongeza serikali kwa kuweka 
mfumo wa kukusanya kodi kwa njia rahisi na yenye uwazi na kufafanua kuwa
wao wamekuwa kampuni ya kwanza kujiunga na kufurahia utaratibu huo kama
ilivyobainishwa na kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), 
Charles Kichere, kwani unawezesha kampuni kuwa wazi katika malipo yote 
ya kodi na tozo wanazozifanya kwa wateja.

Akizungumza 
na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo bwana Le 
Van Dai, amefafanua kuwa wao kama kampuni siku zote wamejiweka mbele  
katika kuhakikisha wanatimiza matakwa ya serikali kwa kufuata taratibu  
zote zinazowekwa na mamlaka husika.

“Tulipofahamishwa 
kuhusu utaratibu huu wa ukusanyaji kodi tulifurahia sana kwa sababu  
unaweka wazi maendeleo ya biashara na ukusanyaji wa mapato ya serikali, 
sisi kama wawekezaji tunafurahia kuwa na njia bora za usimamizi wa  
mapato ya serikali na kampuni husika kwani unatuwezesha sisi pia 
kujipima kujua biashara kama ni nzuri au sivyo na kuangalia namna bora  
ya kushauriana na mamlaka husika katika kufanikisha mazingira bora ya  
kibiashara” Alisema Dai.

Aidha, 
Mkurugenzi huyo pia aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wanaendelea 
kufurahia mafanikio ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiyapata tangu 
kuanzishwa kwake.

“Katika 
taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka huu 2017 iliyotolewa na Mamlaka ya 
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonesha namna ambavyo kampuni yetu 
imeendelea kufanya vyema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita,”

"Kimsingi, 
idadi ya wateja wa kampuni za simu ilipungua kutoka 40,173,783 kwa 
Desemba mwaka jana na kufika39,856,212 kwa Machi mwaka huu. Hii ina 
maana kuwa kuna baadhi ya mitandao ya simu ilipoteza wateja ila Halotel 
tumeweza kuongeza wateja wapya wapatao 73,872. Hii ni ishara kuwa 
Watanzania wanaridhika na huduma zetu. Tunawaahidi kuwa 
hatutawaangusha," alisema,”


Alisema 
Dai na kuongeza kuwa “hii ni dalili nzuri kwetu kibiashara. 
Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kuendelea kujiunga 
na sisi, tunawaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuufanya Halotel
uendelee kuwa Mtandao chaguo namba moja kwao.” Alihitimisha Mkurugenzi 
huyo.

Pamoja 
na mambo mengine Mkurugenzi huyo amesema kampuni hiyo bado inatoa 
kipaumbele kwa kutoa huduma bora kwa jamii ya Watanzania ikiwepo pamoja 
na kuwezesha miundombinu ya mawasiliano kwa taasisi mbalimbali za 
serikali pamoja na taasisi za kijamii, zikiwemo shule, hospitali, ofisi 
za posta na halmashauri mbalimbali. Hivi karibuni kampuni hiyo 
ilitangaza uwekezaji wa Zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha ubora wa 
mtandao huo, ikilenga kuongeza kasi ya intaneti na ubora wa huduma za 
sauti. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages