HAKI ELIMU YAZINDUA KAMPENI ZA UFANIKISHAJI WA ELIMU YA MTOTO WA KIKE - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Wednesday, 21 June 2017

HAKI ELIMU YAZINDUA KAMPENI ZA UFANIKISHAJI WA ELIMU YA MTOTO WA KIKE

SERIKALI  imeelezwa kuwa  kwakiwango  kikubwa mazingira ya kujifunza  na kufundishia  bado si rafiki kwa moto wa kike , kwa mujibu wa takwimu za BEST(BasicUducatin Statics) za mwaka 2016, zimetaja kuwa  kunaupungufu wa mkubwa sana wa matundu ya vyoo  ambapo wasichana 52 wanalazimika  kutumia tundu moja la choo badala ya wasichana  20 kutumia tundu moja la choo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Elimu Nchini , John Kalaghe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuondoa Vikwazo kwa Mtoto wa Kike katika hafla iliyofanyika katika ofsi za Tasisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam Juni 20, 2017.Kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa jamii kumpa fursa msichana hili aweze kupata mafanikio na kufikia maelengo yake (katikati), Msemaji kutoka TGNP, Grace Kisetu .


Ukosefu wa maji pia ni tatizo  kwani  asilimia 43.6 ya shule za msingi  na asilimia 54.4 ya shule za sekondari tu ndiyo zina huduma ya maji, hali ya  ukosefu wa  vyoo  na maji  katika shule ,inahatarisha afya zao na kuwaweka katika  hatari ya kupata magonjwa yohusiana na uchafu.

Akizunguza Dar es Salaam jana kwenye  uzinduzi wa  kampeni  maalumu ya kuhamasisha  ufanikishaji wa elimu ya moto wa kike  Mkurugenzi  Mtendaji wa Hakielimu John Kalage  alisema kuwa kampeni hiyo inatokana na ongezeko  kubwa la changamoto za kimazingira,kiutamaduni,kiuchumi  na kimazoea ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma  sana haki za ya upatikanaji wa elimu bora kwa motto wa kike nchini.

Alisema kuwa   kumekuwepo  na taarifa nyingi za unyanywasaji ambazo kwa kiwango kikubwa mwasilika amekuwa ni motto wa kike, athari za unyanyasaji  huo ni mkubwa na zinahitaji juhudi za pamoja ili kuweza kumkwamua motto wa kikike katika  hatari ya kukosa haki  yake kupata elimu bora na kufikia ndoto  zake  kama mwanadamu na  kama raia yeyote mwingine wa Tanzania.

“Kwa kutambua hilo ,suala la ulinzi  wa motto husuani motto wa kike na wale wenye mahitajia  maalum ni suala ambalo hakielimu imelipa kipau mbele katika  mpango  mkakati wake mpya wa mwaka 2017 hadi mwaka 2021 ambapo kampeni hiyo inachagizwa  na ukweli kuwa elimu ya motto wa kike inachangamoto mali mbali ambazo hazina budi kutatuliwa ili kuwezesha watoto wa kike kuwa shuleni  na kupata elimu bora,”alisema  Kalage.

Kalage alisema  niwazi kuwa  kwa sababu ya maumbile  ya kibaiolojia  motto wa  kike ana mahitaji  zaidi ya  motto wa kiume hata hivyo  kutokana na sababu za kukosa vifaa kama taulo za kike  kwa ajili ya kuwasaidia katika siku  zao,watoto  wengi  wa kike hushindwa kuhudhulia shule  na kuamua  kukaa nyumbani hadi  siku zinapoisha.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa utafiti wa  SNV wa mwaka 2015 umeonesha kuwa asilimia 25 tu wa wasichana  waliohusika katika utafiti  ndio hupata vifaa na kuwa umebainisha kuwa njia madala kwa wasichana  wasiopata  vifaa ni kuamua kukaa nyumbani  kati ya siku 4-5 ili kujisitiri na  kuwepo  aibu.

Alisema uchunguzi wa  HakiElimu kwa  kutumia  takwimu  za BEST takribani  wasichana 700,000 hadi 750,000 wa darasa la sita na saba  hupoteza siku  40 hadi 50 kati ya siku 290 za mwaka  wa masomo ambapo hali hiyo ufanya watoto wake kukosa  vipindi vya kujifunza mada  mambali mbali.
“Ripoti ya Human Rights  Watch ya mwaka 2017 yenye kichwa cha habari(I had aDream to Finish School) imebainisha changamoto lukuki za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto  wa kike kama vile  walimu  kuwataka wanafunzi wa kike  kimapenzi na  kuwavisha kuwaadhibu wanapokataa kufanya mapenzi na walimu,”alisema .

Aidha alisema kuwa unyanyasaji wa wanafunzi wa kike imebainishwa kuwa madhara wanayoyapata watoto wa kike  kwa kufanyiwa  unyanyasaji  na jinsi  unavyo waathiri kisaikolojia na kufanya  washindwe kuzingatia elimu yao wawapo shuleni.

Pia  uhaba wa mabweni na changamoto  za usafiri huwaadhiri pia  watoto wa kike katika elimu ya sekondari, shule nyingi za kata ziko mbali mbali na makazi,ripoti ya HumanRights Watch  ya mwaka 2017 imebainisha kuwa  changamoto za usafiri huwafanya wasichana kulazimika kufanya mapenzi na madereva wa  magari au pikipiki ili kupata urahisi wa kufika ki;la siku shuleni na matokeo yake upata ujauzito na kufukuzwa shule.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337