Header Ads


E-FM YADONDOSHA KAPU LA EID EL-FITRI KWA WASIKILIZAJI WAKE.

 Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
 Makapu ya Eid el-Fitri yakiwa yamesheheni vyakula mbalimbali
 Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
 Mwigizaji mashuhuri  Riyama Ally ambaye ni balozi wa Dstv akimkabidhi mshindi Benjamin n osha kapu lake la Eid el-Fitri’
Meneja wa vipindi wa Efm radio Dickson Mponela akimkabidhi moja ya washindi Rebeca Lukule kapu lake la Eid Al Fitri


Katika kuelekea sikukuu ya Eid el-Fitri, E-FM Radio imetoa zawadi kwa wasikillizaji wake kama ilivyo tamaduni yake ya kutoa kwa jamii, ambapo wasikilizaji 10 kutoka jijini Dare s salaam waliofanikiwa kusikiliza redio na kujibu maswali kuhusu kampeni ya Kapu la sikukuu wameondoka na makapu yalioyo sheheni vitu mbalimbali ikiwemo vyakula muhimu  kwa ajili ya  sikukuu hiyo. 

Tukio hilo limefanyika leo siku ya Jumamosi ya tarehe 24/06/2017 katika ofisi zao zilizopo Kawe – beach.DSTV nao waliongezea nakshi kwenye kapu kwa kuwazawadia washindi wa makapu ya sikukuu ving`amuzi vyao na kuwapa kifurush cha mwenzi moja bure. Zoezi hili litaendeshwa pia kwa washindi kutoka jijini Mwanza ambako EFM Radio inasikika kupitia masafa ya 91.3. washindi hao watajipatia zawadi zao za Kapu la sikukuu siku ya Jumapili tarehe 25/06/217 kwenye ofisi za DSTV Kenyata road Mwanza.
Post a Comment
Powered by Blogger.