WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKARIBISHA MAONI YA WADAU ILI KUPATA SERA MPYA YA UTALI - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 11 May 2017

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKARIBISHA MAONI YA WADAU ILI KUPATA SERA MPYA YA UTALI

 Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga akizungumza na vyombo vya habari juu ya warsha ya siku moja iliyowakutanisha Wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika jana mkoani Iringa  ya kukusanya maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999
 Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Fikira Kisimba (katikati)  akizungumza na  wadau wa Utalii wa Nyanda za Juu  Kusini wakati  alipokuwa akifungua warsha ya siku moja  iliyofanyika mkoani Iringa, Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kulia) akiwa na Mtaalamu Mwelekezi wa zoezi la ukusanyaji maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii kutoka  Economic Social Research and Foundation (ESRF) Prof. Raphael Mwalyosi (kushoto)    
 Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga  akifafanua jambo kwenye warsha ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii iliyofanyika jana mkoani Iringa ambayo iliwakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. 
 Mdau wa Utalii  akichangia maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii katika warsha ya siku iliyowakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika jana mkoani Iringa 
 Mdau wa Utalii  akichangia maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii katika warsha ya siku iliyoowakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika mkoani Iringa 
 Baadhi ya Wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu wakifuatilia mjadala wa utoaji maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 katika warsha iliyofanyika jana mkoani Iringa  
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu wa Mkoa wa Iringa, (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Utalii wa Nyanda za Juu Kusini  mara baada ya kufungua mkutano wa kukusanya maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 kwenye warsha iliyofanyika jana Mkoani Iringa. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kulia) akiwa na Mtaalamu Mwelekezi wa  Economic Social Research and Foundation (ESRF) Prof. Raphael Mwalyosi (kushoto) pamoja na Prof. Amosi  Majule     (Picha na Lusungu Helela-MNRT
.....
Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka Wadau wa  Sekta ya  Utalii wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutoa maoni na michango yenye tija itakayopelekea upatikanaji wa Sera Mpya ya Utalii.

Sera hiyo   inatarajiwa kutoa  majibu ya changamoto za utalii wa sasa kwa sababu itagusia  utalii nje ya hifadhi.

Kauli hiyo imekuja baada ya  Sera ya Taifa ya Utalii inayotumika hadi hivi sasa kufanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka 17 iliyopita. 
Hayo yameibainika kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kuwatanisha wadau wa sekta hiyo wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili kukusanya maoni ya upungufu na utekelezaji wake.

Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga alisema Sera na miongozo inayoongoza Sekta ya utalii imepitwa na wakati kutoka na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyotokea mfano, Serikali kujiondoa katika umiliki na uendeshaji wa huduma za kitalii na kuachia sekta binafsi.

’’Si hayo tu sera ya awali haikuainisha vivutio vyote vya utalii zaidi ya hifadhi pekee ambapo kwa sasa tatizo la ujangili na mabadiliko ya tabia nchi yameathiri kwa kiasi kikubwa’’ alisema

Aliongeza kuwa, Sera mpya itakayoundwa itaweza kwenda sambamba na aina ya utalii wa sasa ambao kipindi cha nyuma haukuwepo, akitolea mfano utalii mikutano pamoja na utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukikua kwa kasi hapa nchini

Aidha, alifafanua kuwa wanahitaji miongozo mipya itakayosimamia sekta hiyo ili kuondoa migongano ya kiutendaji katika taasisi zinazohusika ikiwemo ya wanyamapori, misitu na uwekezaji ili kuendeleza utalii na sio kudidimiza.

Akifungua warsha hiyo, Kaimu  Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Fikira Kisimba  allisema wameamua kupitia sera hiyo kutokana na kasi ndogo ya maendeleo yanayopatikana katika sekta hiyo licha ya kujaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii.

Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Mkoa wa Njombe, Amiri Abdi, alisema sera itakayoundwa iangalie namna ya kuweza kutumia teknolojia rafiki  ya kuvitangaza vivutio vya vya Utalii vya Nyanda za Juu Kusini kwa kutumia gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages