WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YATOA UJUMBE WA TAHADHARI KATIKA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI – MEIMOSI - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 1 May 2017

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YATOA UJUMBE WA TAHADHARI KATIKA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI – MEIMOSI

    Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kanda ya Kaskazini wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi – Kilimanjaro.
 Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
   Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam wakijipanga kuanza maandamano rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi –  viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam (Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi) wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
    Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam wakifurahi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Meimosi yakiendelea – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kutahadharisha umma kuhusu umuhimu wa ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati, katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi mkoani Moshi, ambapo sherehe hizo zimeazimishwa rasmi kitaifa.  Na Dar es Salaam katika viwanja vya Uhuru.

Kutokana na Wizara kuendelea kuwahimiza Wamiliki wa Ardhi kulipa kodi ya pango la Ardhi, Watumishi hao wameona ni wakati muafaka kuendelea kutangaza ujumbe huo kwa mabango katika kuadhimisha sherehe za Meimosi. 

Aidha, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Mhe. William Lukuvi amesema; ambaye hajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, alipe kabla ya mwisho wa mwezi wa sita (6), kwakuwa ifikapo tarehe 30/06 hatua zifuatazo zitachukuliwa dhidi yao; 

Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao zitakamatwa na majengo yatapigwa mnada kupitia madalali na Miliki zao zitafutwa kwa mujibu wa Sheria.

Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages