TUANAAMINI KUWA MVUA NZURI NA YA BARAKA HUTOKA KWA MUNGU -DKT. CHARLES GADI - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 11 May 2017

TUANAAMINI KUWA MVUA NZURI NA YA BARAKA HUTOKA KWA MUNGU -DKT. CHARLES GADI

 Askofu Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam w akitoa  pole kwa vifo vya wanafunzi waliopata ajali Karatu Mkoani Arusha hivi karibuni.
Angalia video
Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry ya jijini Dar es Salaam, Dkt. Charles Gadi kwa kushirikiana na maaskofu wenzake wamefanya maombi ya  kuwaombea wanafunzi waliokumbwa na mauti huko mkoani Arusha.

Amesema Taifa limepatwa na pigo kubwa kwa kuondoka kwa wasomi hao wa kesho ambao idadi yao ni kubwa kwa wanafunzi  32, walimu wawili na dereva wa basi lililowabeba wanafunzi wa shule hiyo ya msingi Lucky Vicent ya jijini Arusha.

Askofu Gadi amewataka wazazi na taifa kwa ujumla wawe na moyo wa subira wakati huu mgumu wa majonzi na kusema watanzania wanapaswa kuungana na familia hizo kuwaombea watoto hao. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Askofu Dkt. Gadi amesema, mvua zinazoendelea kunyesha sio mvua ya mwenyezi mungu bali ni mvua ya shetani.

Amesema, mvua ya mwenyezi mungu hua madhara ambayo yatasababisha maafa kwa sababu mungu alisema hawezi kuangamizwa watu wake kwa maji ndio maana aliweka ukingo (Raimbow).

"Vilevile tuanaamini kuwa mvua nzuri na ya baraka hutoka kwa mungu lakini inapoanza kuzidi na kuharibu madaraja nyumba, barabara, kuua watu, mifugo na kuharibu mashamba huo unakuwa sio mkono wa mungu, kwani mvua ni baraka kutoka mungu lakini hachanganyi huzuni naye" amesema Askofu Dkt. Gadi.

Aidha aliongeza kuwa, hivyo tunamuomba mungu mvua ziendelee kuwa baraka na msaada kwa nchi yetu na watu wake, ndio maana tunakwenda kuomba mvua zihamie kule mikoani ambapo bado mazao yake ni machanga na yanahitaji mvua zaidi ili yakomae, amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages