SBL YATOA SH.BILIONI 2.1 KUIDHAMINI TAIFA STARS KWA MIAKA MITATU - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Breaking

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222

Post Top Ad

Post Top Ad


Saturday, 13 May 2017

SBL YATOA SH.BILIONI 2.1 KUIDHAMINI TAIFA STARS KWA MIAKA MITATU

 Mkataba ukioneshwa baada ya kusainiwa.
Mfano wa hundi yenye thamani ya sh.bilioni 2.1 ikioneshwa kwa wanahabari baada ya SBL kuikabidhi kwa TFF.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNIya Bia Serengeti (SBL) imeingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF)  wathamani ya  shilingi bilioni 2.1  ambao unaifanya kuwa mdhamini  mkuu  wa timu ya taifa-Taifa Stars.

 Hii ni mara ya pili kwa SBL  kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.

Katika  makubaliano hayo  ambayo  yalisainiwa jijini Dar es Salaam  jana na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata  fursa ya kutangaza biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.

Akizungumza  wakati wa kusainiwa  kwa mkataba  huo  Weesie   alisema  uamuzi  wa  kampuni  hiyo wa kuidhamini  timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya  kusaidia  kuleta  maendeleo  katika sekta mbalimbali za ijamii ikiwemo michezo. 

Alisema wanaunga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba  michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.

“SBL  inaona  fahari  kuidhamini  timu yetu ya taifa kwa mara nyingine  tumechukua  hatua  hii  kwa  kuwa  tunaelewa  mchango  wa  sekta  ya  michezo  katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii " alisema. 

Aidha  Weesie aliongeza kuwa wanaamini  kuwa  udhamini  wao huo utachangia  kukuza  vipaji  vya  vijana  wetu  pamoja  na  kuleta  hamasa  kubwa  kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa.

Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo  ambalo  alisema  litasaidia  katika  kufanikisha  maandalizi  mazuri  na  ushiriki  kikamilifu  wa timu hiyo katika  mashindano mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

“Udhamini  wa SBL  umekuja kwa wakati mwafaka,  wakati  ambapo timu yetu ya taifa ipo katika  hatua za   maandalizi  kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.

Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo  ilihudhuriwa na Waziri wa Habari,   Utamaduni Sanaa na Michezo  Dk.Harisson Mwakyembe ambaye  alitoa wito kwa   kampuni  zingine  na  watu  binafsi  wenye  mapenzi  na  michezo  kujitokeza  na  kutoa  michango  ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.No comments:

Post Top Ad

Tangaza nasi Hapa-+255787 942 222