Header Ads


RC TABORA AWATAKA WATOA HUDUMA KATIKA MACHIMBO YA KITUNDA ZINGATIENI USAFI

Na Tiganya Vincent, Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri awaagiza wafanyabiashara wote walioko katika eneo la machimbo ya dhahabu Kitunda wilayani Sikonge kuhakikisha wanakuwa na maeneo ya kuhifadhi taka ngumu na laini kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya mlipuko.

Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo  jana wilayani humo wakati anaongea na wakazi wa Kitunda wanajihusisha na uchimbaji wa dhahabu au utoaji wa huduma za vinjwaji na chakula machimboni hapo.

Alisema kuwa hakuna hatakayeruhusiwa kuendesha shughuli zake mbalimbali ziwe za uchimbaji au biashara chakula na vinjwaji kama hatakuwa amechimba choo na kuweka kifaa cha kutupa mabaki ya taka ngumu na laini.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa eneo hilo linahitaji usafi wa hali ya juu kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambapo inaweza kusababisha maafa itatokea mtu mmoja akaugua ugonjwa wa mlipuko kama vile kipindupindu aliweza kuwaathiri watu wengi na wakati mwingine kusababisha maafa ambayo yanaweza kuzuilika.

"Hapa lazima tuhakikishe usafiri wa hali ya juu kwani tusipofanya hivyo tunaweza kufa kama kuku waliougua ugonjwa wa kideli ...uongozi huu hako tayari kuona mtu anafanyabiashara katika mazingira hatarishi kwa wateja wake"alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha , Mkuu huyo wa Mkoa aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuleta Pipa kubwa la kutupa taka ili kulinda mazingira ya eneo hilo.

Kwa upande wa wachimbaji wa eneo hilo amewaagiza kujiwekea taratibu za kutozana faini kwa watu wanachafua mazingira kwa ajili ya kuhakikisha afya zinaendelea kuwa salama na magonjwa ya mlipuko na hivyo kuendelea na shughui za uchimbaji madini pindi watakaporuhusiwa.

No comments

Powered by Blogger.