RC ASIYETAKA KUPANDA MITI ANA SIFA YA KUKAA TABORA - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 27 May 2017

RC ASIYETAKA KUPANDA MITI ANA SIFA YA KUKAA TABORA

Na Tiganya Vincent, Sikonge
Serikali ya Mkoa wa Tabora imesema mkazi wake anayepinga zoezi la upandaji miti katika maeneo yake ni vema akatafuta sehemu nyingine ambayo hawako tayari  kuhifadhi mazingira.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Bw. Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano wa hadhara wilayani Sikonge alipokuwa akiwaelimisha juu ya zoezi linaloendelea mkoani humo la kupanda miti ili kukabiliana na uharibifu wa mistu uliosababishwa na shughuli mbali za binadamu.
Alisema kuwa Mkoa wa Tabora unanyewelewa kugeuka kuwa Jangwa kama juhudi zisipofanyika mapema kutokana na ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya nishati ya kukaushia tumbaku , matumizi ya majumbani, ujenzi na ufugaji wa kuhama hama ambao hauzingatia utunzaji bora wa mazingira.
Bw. Mwanri aliongeza kuwa mtu au kikundi chochote kitakachokaidi zoezi hilo la kukarabati upya uoto wa asili na upandaji wa miti katika Mkoa wa Tabora , kitakuwa hakiwataki mema wananchi .
Alisisitiza uharibifu uliofanyika umesabibisha upungufu mkubwa wa mvua katika mkoa huu na kufanya vyanzo vingi vya maji kukauka na hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wake.
Mkuu huyo Mkoa alisema suala la kupanda miti ni la wakazi wote wa Tabora na sio la  viongozi wa Serikali, mashirika ya umma , wanafunzi  na dini pekee.
Aliongeza kuwa kipindi hiki ndio kizuri cha kupanda miti kwani ikimwagiliwa vizuri kwa kutumia teknolojia ya matone na wakati ikigonja mvua haitakufa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Simon Ngatunga alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora ,kuwa wao wamenunua miti maji 5078 na kilo 38 za miti kutoka mkoani Dodoma kwa lengo la kupanda na kuzalisha miche zaidi 10,000 ili kuendeleza zoezi hilo la upandaji miti.
Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha mitaa yote ya Halmashauri ya Wilaya hiyo inakuwa na miti kwa ajili ya kuupamba mji wa Sikonge na utunzaji wa mazingira.
Bw. Ngatunga alitoa wito kwa wananchi ambao miti imepandwa katika maeneo ya shughuli zao mbalimbali ikiwemo biashara kuhakikisha wanaitunza miti hiyo kwa kuimwagiliaji ili isije ikafa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages