MEI MOSI SHINYANGA -YAFANA - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 2 May 2017

MEI MOSI SHINYANGA -YAFANA

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wafanyakazi wakati wa kilele cha Siku ya Wafanyakazi kimkoa ambayo ilifanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
 Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali la Mitaa (TALGWU) wakiwa katika maandamano kuingia uwanjani.
 Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (wa pili kushoto) akifuatilia maandamano ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali walipokuwa wakipita mbele yake. Wengine pichani kuanzia kulia ni KatibuTawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabanga Taraba, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.
 Gari la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa likiongoza magari ya taasisi zingine kupita mbele ya mgeni rasmi na wafanyakazi kuonesha shughuli zinazofanya wakati wa sherehe za Mei Mosi.
 Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wakiwa katika maandamano.
 Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (wa tatu kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro (wa pili kulia) wakiserebuka muziki aina ya  kwaito pamoja na wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali.
 Wafanyakazi kutoka halmashauri mbalimbali mkoani Shinyanga wakishindana kuvuta kamba ikiwa ni mojawapo ya burudani wakati wa sherehe hiyo.
 Sehemu ya wafanyakazi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
MEI MOSI SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amewataka wafanyakazi kutumia fursa zilizopo kwa kujituma katika uzalishaji ili kupata malighafi zitakazotumika katika viwanda.

Telack alitoa rai hiyo juzi kwa wafanyakazi mbalimbali mkoani hapa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kimkoa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kambarage.

Alisema wafanyakazi mbali ya kufanya kazi za kuajiriwa pia wana nafasi ya kujiendeleza kwa kilimo cha mazao mbalimbali ili viwanda vyetu vipate malighafi ya kutengenezea bidhaa.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri kila mfanyakazi akiweza angalau awe na ekari moja kwa ajili ya kilimo badala ya kutegemea tu mshahara wa mwisho wa mwezi hali itakayochangia uchumi wa viwanda.

Aliwaagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya waweke mkakati wa kuwapatia watumishi wao maeneo ili waweze kutumia fursa ya kufanya kilimo kuwa sehemu ya kazi.

Mbali ya kuwapongeza wafanyakazi, kwa upande mwingine, Telack aliwataka watumishi wajenge utamaduni wa kuheshimian katika maeneo yao ya kazi na kuepuka migogoro isiyo na tija ili kuleta ufanisi katika kazi.

Aliwaagiza waajiri wa sekta binafsi kutatua kero za wafanyakazi wao ndani ya wiki mbili na kuhakikisha wanatekeleza maagizo yanayotolewa na Serikali kuhusu sekta ya ajira.

Telack alibainisha kuwa akishirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa ataunda kamati sekta binafsi zote zenye changamoto kwa wafanyakazi wao kuhakikisha kuwa zinazitatua mara moja.   

Pia alivitaka vyama vya wafanyakazi viwe sehemu ya kutetea wafanyakazi na si kugeuka kuwa wanaharakati hali inayoweza kuchangia migogoro na waajiri wao.

Sherehe hizo zilizoambatana na maandamano ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali pamoja na burudani zilihudhuriwa pia na wakuu wa wilaya za mkoa huo, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na viongozi wengine mbalimbali.

Sherehe hizo kitaifa kwa mwaka huu zilifanyika mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais John Magufuli zikiwa na kaulimbiu ‘Uchumi wa viwanda uzingatie haki, maslahi na hesma ya wafanyakazi’.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages