MANISPAA YA TABORA YATAKIWA KUWAONDOA WAUUZA MITI WANAOPANGA NGUO MITI YA MITAANI. - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 29 May 2017

MANISPAA YA TABORA YATAKIWA KUWAONDOA WAUUZA MITI WANAOPANGA NGUO MITI YA MITAANI.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt .Thea Ntara .
Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt .Thea Ntara ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora na Maafisa Biashara kuhakikisha wanawaondoa haraka wafanyabiashara wote waliotundika nguo za mitumba katika miti kwa ajili ya kuuza na kufanya mji kuonekana mchafu.
Dkt. Ntara alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao na Wakuu wa Idara  wa Ofisi yake.
Alisema kuwa hivi sasa mji unaonekana mchafu kwa sababu ya baadhi ya wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika mitaa mingi ya Manispaa hiyo kuamua kuweka bidhaa zao katika miti kama mahali rasmi pa kufanyia biashara hiyo.
Dkt.Ntara aliongeza kuwa ni vema Uongozi wa Manispaa ya Tabora wakahakikisha wanatenga maeneo maalum ya vijana hao kuendesha kazi zao badala ya kuwaacha wafanyebiashara kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
“Haiwezekani kila mahali kwenye miti kunageuzwa sehemu ya kuuzia mitumba …ni lazima mji ukae katika utaratibu na mpangilio unaofaa” alisema Katibu Tawala huyo wa Mkoa.
Alisisitiza kuwa miti iliyopo mitaani ni kwa ajili ya kusaidia kutunza mazingira na kusaidia  kivuli kwa wapita njia na sio ya kupanga na kuuzia nguo za mitumba.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora ameuagiza Uongozi wa Manispaa hiyo kutenga haraka eneo la kuchimba vyoo kwa ajili ya wafanyabiashara wa Mnada wa eneo la Ipuli ili kuzuia watu kusaidia ovyo katika eneo hilo.
Alisema kuwa kama watashindwa kutekeleza agizo hilo atalazimika kusimamisha shughuli za biashara ili kuzuia uwezekano wa kuzuka magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu ambayo yanaweza kusababisha maafa.
Dkt. Ntara alisisitiza kuwa haiwezekana huduma mbalimbali kama vile uuzaji wa vyakula, nyama choma na bidhaa nyingine zikafanyika katika eneo ambalo halina huduma ya vyoo kwa ajili ya watu wanakwenda kununua na kuuza bidhaa mbalimbali.

Alitoa wiki moja kuhakikisha zoezi hilo linafanyika la sivyo hatachukua hatua ya kusimamisha shughuli katika eneo hilo hadi hapo watakapoboresha na kujenga vyoo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages