Habari za sasa hivi

MAMBO KADHAA KUHUSU WATOTO WA KIKE NA ELIMU | FACTS ABOUT GIRLS’ EDUCATION

 Zaidi ya wananchi 7 kati ya 10 wanataka wasichana waendelee na shule iwapo watapata ujauzito

Kwa mujibu wa ripoti ya UNFPA kuhusu mimba za utotoni, utafiti uliofanyika kwa wanawake wenye miaka kati ya 20-24 nchini Tanzania unaonyesha kuwa asilimia 28 yao walijifungua kabla ya umri wa miaka 18.

Matokeo yake ni kuwa idadi kubwa ya wasichana waliacha shule kutokana na tatizo hili. Hatahivyo,
Tanzania haina sera inayowaruhusu wasichana wanaopata mimba kurudi shuleni. Wananchi walipoulizwa kuhusu suala la wasichana kupata ujauzito wakiwa shule, asilimia 21 ya wananchi walisema kuwa wanafahamu familia ambayo mwanafunzi aliyeacha shule ya msingi au sekondari kutokana na ujauzito.

Miongoni mwa wale wanaofahamu wanafunzi kama hawa, asilimia 72 wanasema wanafunzi hao walibaki kuwa mama wa nyumbani.

Walipoulizwa mtazamo wao juu ya hili, wananchi 6 kati ya 10 (asilimia 62) walijibu kuwa wangependa wanafunzi hao waruhusiwe kurudi shule baada ya kujifungua na asilimia 21 walisema waondolewe shuleni moja kwa moja.