DC SIKONGE AAGIZWA KUSIMAMIA ZOEZI LA UFUKIAJI WA MASHIMO AMBAYO HAYAKUFUATA UTARATIBU. - Mtazamo News
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 26 May 2017

DC SIKONGE AAGIZWA KUSIMAMIA ZOEZI LA UFUKIAJI WA MASHIMO AMBAYO HAYAKUFUATA UTARATIBU.

Na Tiganya Vincent

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Sikonge kusimamia zoezi la uhakiki vya upimaji na ufukiaji wa mashimo yote ambayo hayakuzingatia vipimo vinavyotakiwa katika shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo la Kitundi wilayani Sikonge ili kuepusha maafa.

Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge baada ya kutembelea machimbo ya Kampuni ya Kapumpa Gold Mining ili kuangalia jinisi walivyotekeleza maagizo mbalimbali ya Serikali .

Baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukagua na kuendesha zoezi la uhakiki wa umbali wa shimo moja kwenda jingine alibaini kuwa ni kweli baadhi ya mashimo yalifukiwa wakati waliposikia anatembelea eneo hilo.

Alisema kuwa ni vema mashimo yakazingatia umbali unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za uchimbaji madini mdogo mdogo ili kuepusha vifo vinavyoweza kusababishwa na umbali toka shimo moja hadi jingine kuwa karibu sana.

Bw. Mwanri alisema kuwa haiwezekana Serikali iagize Kampuni hizo zingatie vipimo katika upangaji wa mashimo , halafu wenyewe wajingie vipimo kama wanavyotaka bila kuchukua tahadhari ya maisha ya wachimbaji hao.

Alisema kuwa zoezi hilo la ufukiaji ni vema likaanzia chini na sio kama walivyoweka miti na nyasi mithili ya mtu aliyetengeneza choo cha kienyeji ambapo miti ikioza unaweza kusababisha mtu kutumbukia ndani na kuleta maafa mengine.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa ufukiaji usiozingatia utalaam ndio unaozifanya kampuni hizo zitoe miti wakati viongozi hawapo katika eneo hilo na kuendeleza uchimbaji ambao ni hatarishi.

Awali wachimbaji wawili wadogo wadogo ndio waliofichua uovu na udanganyifu huo uliofanywa na Kampuni ya Kapumpa ya kufikia mashimo baada ya kusikia Mkuu huyo wa Mkoa alitembelea eneo hilo.

Wachimbaji hao walimpeleka Mkuu huyo wa Mkoa toka shimo hadi jingine lilikuwa likichimbwa kinyume cha utaratibu na kulifukia baada ya kusikia ziara ya kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages