Habari za sasa hivi

WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS AFUNGA WARSHA YA SIKU TANO YA KUTATHMINI KANUNI ZA AFYA ZA KIMATAIFA ZANZIBAR

 Mgeni rasmin Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud akifunga warsha ya siku tano ya kutathmini kanuni za Afya kimataifa Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Ocen View Kilimani Mjini Zanzibar. 
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dk. Ghirmany Andermichal akitoa tarifa ya shirika hilo katika warsha ya siku tano ya kutathmini kanuni za Afya kimataifa iliyofanyika Hoteli ya Ocen View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Kiongozi wa warsha ya kutathmini kanuni za Afya kimataifa kutoka (WHO) AFRO Dk. Ambrose Jalisuna akitoa muhtasari wa taarifa ya awali ya tathmini waliyoifanya Zanzibar. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla akimkaribisha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud kufunga warsha ya kutathmini kanuni za afya kimataifa katika ukumbi wa Hoteli ya Ocen View, (kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dk. Ghirmany Andermichal.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya kutathmini kanuni za Afya kimataifa wakifuatilia ufungaji wa warsha hiyo.


Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.