Header Ads


PRO KABUDI AZINDUA TAARIFA YA HAKI ZA BINADAMU KWA MWAKA 2016

Serikali imewahakikisha watetezi wa haki za binadamu nchini kuwa serikali inatambua mchango walionao katika kuhakakisha haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa nchini na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao na kuwawekea mazingira stahiki ya watetezi wa haki za binadamu kuendelea kufanya kazi zao kwa utimilivu.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof  Palamagamba Kabudi mjini Dar es salaam katika maadhimisho ya Nne ya watetezi wa haki za binadamu nchini kwa niaba ya Makamu wa Rais mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika maadhimisho hayo Prof Kabudi alizindua taarifa ya hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2016 ambayo iliandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.

Maaadhimisho hayo yameandaliwa na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini na kuhudhuriwa na watetezi wa haki za binadmu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia yamehudhuriwa na wawakilishi wa malozi na mashirika ya kimataifa, Wizara na taasisi za serikali Maadhimisho hayo ya mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo kuboresha ushirikiano na serikali

No comments

Powered by Blogger.