BAADHI YA WATUMISHI WANAKWAMISHA ZOEZI LA KUONDOA VIPOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU-RAS TABORA. - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 21 April 2017

BAADHI YA WATUMISHI WANAKWAMISHA ZOEZI LA KUONDOA VIPOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU-RAS TABORA.

Na Tiganya Vincent-RAS-Tabora

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amesema kuwa zoezi na kukabiliana na wauzaji wa dawa na vipodozi vilivyopigwa marufuku limekuwa likikwamishwa na baadhi ya watumishi  wasio waaminifu na wasiozingatia maadili ya kazi zao kwa kuvujisha siri za kusudio la kufanya zoezi la ukaguzi na hivyo kuwafanya wahusika wafiche bidhaa hizo ili wasikamatwe.

Hali imefanya bidhaa hizo kuendelea kutumiwa na baadhi ya wananchi na hivyo kendelea kuathiri afya zao na nguvu kazi ya Taifa.

Dkt. Ntara ametoa kauli hiyo leo mjini Tabora wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uelimishaji Umma kwa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo mkoani hapa juu usimamizi wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura 219 ili kulinda jamii na matumizi ya  ipodozi vilivyopigwa marufuku.

Amesema kuwa ili kukabiliana na chanagamoto hiyo ni vema  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ikaendesha zoezi la kushitukiza la mara kwa katika maduka ya vipodozi ili kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiendelea kuuza dawa na vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Dkt. Ntara amesema kuwa msako wa kushitukiza utasaidia kuwabaini wafanyabiashara wote wanaoficha bidhaa zao baada ya kupewa taarifa ya watumishi wasio waaminifu na hivyo kuwachukulia hatua ili kulinda jamii isiendelea kuathirika na matumizi hayo.

Aidha, Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora alitoa wito kwa wanafunzi na wanachuo wote mkoani humo kutumia elimu waliyopatiwa na TFDA kudhibiti matumizi na vipodozi vilivyopigwa marifuku na kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara yanayosababishwa na matumizi ya vipodiozi hivyo.

Amesema kuwa ni vema mabinti wakatambua kuwa kubadilisha ngozi zao sio urembo bali kukalibisha madhara makubwa yatakayowapata siku za usoni.

Dkt. Ntara amesema kuwa watu wote watakaozingatia elimu hiyo watakuwa na kizazi kisichokuwa na athari ya vipodozi.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa Mamlaka hiyo katika kuhakikisha kuwa jamii kubwa inapata elimu juu ya athari za matumizi ya chakula , dawa na vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya binadamu , tayari wameshaendesha mafunzo kwa washiriki 64,479.

Amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo ni wanahabari, walimu, wanafunzi, wajasiriamali na watumishi mbali mbali ikiwa lengo ni kuhakikisha kuwa kundi hilo nalo linasaidia kutoa elimu kwa umma juu ya athari za vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa lengo la elimu hiyo ni kutaka kundi hilo lisaidie kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari mapema ili waweze kuepuka matumizi ya vipodozi visivyofaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages